Iran yasitisha rasmi ushirikiano wake na shirika la IAEA
2 Julai 2025Sheria hiyo inasema ukaguzi wowote utakaofanywa na IAEA katika vinu vya nyuklia vya Iran ni lazima kwanza uidhinishwe na Baraza la Juu la Usalama wa Taifa nchini humo. Hata hivyo IAEA imekiri kufahamu hatua iliyochukuliwa na Iran na imesema inasubiri taarifa zaidi kutoka huko.
Iran yasitisha rasmi ushirikiano na IAEA
Iran ilitishia kusimamisha uhusiano na IAEA baada ya kuishutumu kuegemea mataifa ya Magharibi na kuhalalisha mashambulizi ya Israel dhidi ya taifa lake, yaliyoanza siku moja baada ya bodi ya shirika hilo kwa pamoja kusema Jamhuri hiyo ya kiislamu inakiuka makubaliano ya mkataba wa Kuzuia kusambaa kwa silaha za nyuklia (NPT).
Awali waziri wa mambo ya kigeni wa Iran Abbas Araqchi alikiambia kituo cha televisheni cha Marekani cha CBS kwamba mashambulizi ya Washington dhidi ya kinu chake muhimu cha nyuklia cha Fordow yalikiharibu vibaya kinu hicho.