SiasaIran
Iran yashutumu vitisho vya Ufaransa juu ya kurejesha vikwazo
30 Aprili 2025Matangazo
Hayo yameripotiwa na vyombo vya habari vya Iran vilivyonukuu barua iliyotumwa na ujumbe wa Jamhuri hiyo ya Kiislamu katika Umoja wa Mataifa.
Sehemu ya barua hiyo iliyochapishwa na shirika la habari la Iran, ISNA imeeleza kuwa, nchi hiyo kamwe haitakubali vitisho.
Soma pia: Iran: Duru ya pili mazungumzo na Marekani itafanyika Roma
Kauli hiyo ya Iran imetolewa baada ya Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Jean-Noel Barrot kusema siku ya Jumatatu kwamba serikali yake kwa ushirikiano na Ujerumani na Uingereza, hazitasita hata kwa sekunde moja kurejesha vikwazo vyote vilivyoondolewa miaka kumi iliyopita iwapo usalama wa Ulaya utatishiwa na shughuli za nyuklia za Iran.