Iran: Mazungumzo yalikuwa "magumu lakini yenye manufaa"
12 Mei 2025Hata hivyo, pande zote mbili – Tehran na Washington, zimethibitisha mipango ya kuendelea na mazungumzo zaidi katika siku zijazo.
Hii ilikuwa duru ya nne ya mazungumzo yaliyoanza karibu mwezi mmoja uliopita, ikiwa ni ishara ya mazungumzo ya ngazi ya juu zaidi kati ya mahasimu hao mawili tangu Marekani ilipojiondoa kutoka makubaliano ya kihistoria ya nyuklia mnamo mwaka 2018, wakati wa muhula wa kwanza wa Rais Donald Trump.
Soma pia: Iran yatetea haki yake ya kurutubisha madini ya Urani
Pande zote mbili zimeripoti maendeleo katika duru tatu zilizopita, na jana Iran ilisema mkutano huo ulikuwa "mgumu lakini wenye manufaa” na kwa upande wa Marekani, afisa mwandamizi wa Washington akieleza kuwa nchi hiyo "imetiwa matumaini.”
Afisa huyo, akizungumza kwa masharti ya kutotajwa jina, amesema Marekani imetiwa matumaini na matokeo ya mkutano huo na kwamba anatarajia kufanyika kwa mkutano mwengine ambao utafanyika hivi karibuni, bila ya kutoa tarehe maalum.