SiasaIran
Iran yasema mazungumzo ya kwanza na Marekani yalienda vizuri
15 Aprili 2025Matangazo
Lakini Khamenei ameelezea imani yake na msimamo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wa kutilia mashaka nia halisi ya Marekani.
Kiongozi Mkuu wa Iran mwenye umri wa miaka 85 amesema mazungumzo kati ya nchi yake na Marekani yalifanyika vyema katika hatua za kwanza. Hata hivyo ameeleza kuwa Iran inayo mashaka makubwa kuhusu upande mwingine, lakini amesema anayo matumaini juu ya uwezo wa Iran. Kwa mujibu wa televisheni ya taifa, maoni ya kiongozi huyo Mkuu wa Iran, japo yametolewa kwa uangalifu mkubwa yanaashiria kuyaunga mkono mazungumzo hayo na Marekani juu ya mpango wa nyuklia wa Iran.