Mazungumzo ya Iran na Marekani kuhusu nyuklia yafanyika Oman
12 Aprili 2025Msemaji wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Esmail Baghaei kupitia mitandao ya kijami amesema majadiliano aliyosisitiza kuwa yasiyo ya moja kwa moja yamefanyika kwa maafisa wa Oman kupeleka ujumbe kwa pande zote.
Majadiliano hayo ni harakati mpya za kufufua juhudi za kidiplomasia wakati kukiwa na mivutano inayoendelea kuhusu shughuli za kinyuklia za Iran.
Soma zaid: Majadiliano kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran yanafanyika nchini Oman
Waziri wa mambo ya Kigeni wa Iran Abbas Araghchi ameiwakilisha Tehran kwenye mazungumzo hayo na mjumbe maalumu wa Marekani Steve Witkoff amemuwakilisha Rais Donald Trump.
Shirika la habari la Iran limeripoti kuwa awamu hii ya mazungumzo imekamilika. Mazungumzo hayo ambayo Iran imesema yalikuwa mazuri na yenye tija, yamepangwa kuendelea wiki ijayo.