Iran yasema iko tayari kwa mazungumzo ya nyuklia
30 Januari 2025Kulingana na Baqaei, kwa mara kadhaa wamesema wako tayari kwa mazungumzo, lakini ikiwa tu upande wa pili uko makini kuhusu suala hilo.
Katika mahojiano hayo, Baqaei ameelezea matumaini yake kwamba Rais mpya wa Marekani Donald Trump atazingatia mtazamo wa kweli kuelekea Iran.
Baqaei asema sera ya Iran itategemea vitendo vya wahusika
Alipoulizwa kuhusu uwezekano wa duru mpya ya mazungumzo, Baqaei alinukuliwa akisema kuwa sera ya Iran itategemea vitendo vya wahusika wengine.
Shirika la IAEA limeitaka Iran kushirikiana haraka na kikamilifu
Hata hivyo, ameonya kuwa ikiwa hilo litatokea, uzingatiaji wa Iran kwa Mkataba wa Kuzuia Kuenea kwa Silaha za Nyuklia, NPT hautakuwa tena na maana yoyote.
Araghchi asema Marekani inapaswa kurudisha imani ya Iran
Katika mahojiano na Sky News yaliyochapishwa katika kituo chake rasmi cha Telegram siku ya Jumanne, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi, alisema utawala mpya wa Marekani unapaswa kufanya kazi ili kurudisha imani ya Iran ikiwa inataka duru mpya ya mazungumzo ya nyuklia.
Hivi karibuni, Iran ilitoa ishara kwa nchi za Magharibi mara kadhaa ikionyesha nia ya kufikia makubaliano kuhusu mpango wake wa nyuklia.
Trump alifuata sera ya shinikizo kali
Wakati wa muhula wake wa kwanza madarakani uliomalizika mnamo 2021, Trump alifuata sera ya shinikizo kali, na kuiondoa Marekani kutoka kwenye makubaliano ya kihistoria ya nyuklia kati yaIran na mataifa sita yenye nguvu duniani ambayo yaliweka vikwazo katika mpango wa nyuklia wa Iran kwa kubadilishana na kupunguzwa kwa vikwazo.
Iran ilizingatia makubaliano hayo yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) hadi mwaka mmoja baada ya Marekani kujiondoa katika makubaliano hayo mwaka 2018, lakini ikaanza kupunguza kujitolea kwake. Tangu wakati huo, juhudi za kuufufua mpango huo wa nyuklia wa mwaka 2015 hazijafua dafu.
Rais Pezeshkian atoa wito wa kukomeshwa kutengwa kwa nchi yake
Mara kwa mara, Iran imeelezea nia ya kuyafufua makubaliano hayo ya nyuklia, na Rais Masoud Pezeshkian, ambaye alichukua madaraka mwezi Julai mwaka jana, ametoa wito wa kukomeshwa kutengwa kwa nchi yake.
Iran ilifanya mazungumzo na Uingereza, Ufaransa na Ujerumani
Kabla ya Trump kurejea madarakani, maafisa wa Iran walifanya mazungumzo ya nyuklia na washiriki wao kutoka Uingereza, Ufaransa na Ujerumani ambayo pande zote mbili ziliyataja kuwa ya wazi na yenye tija.
Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zaishtumu Iran
Mnamo mwezi Desemba, serikali hizo tatu za Magharibi ziliishutumu Iran kwa kuongeza hifadhi yake ya madini ya urani yaliyorutubishwa kwa kiwango cha juu mno bila ya uhalalishaji wa kuaminika wa kiraia na kujadili uwezekano wa kurudisha vikwazo.
Mazungumzo ya nyuklia na Iran kuendelea Vienna
Chini ya Mkataba wa Kuzuia Kuenea kwa Silaha za Nyuklia, NPT, mataifa yaliyotia saini yanalazimika kutangaza hifadhi zao za nyuklia na kuziweka chini ya usimamizi wa Shirika la Kimataifa la Kudhibiti nishati ya nyuklia la (IAEA).