Iran: Tuko tayari kwa mazungumzo ya haki kuhusu nyuklia
29 Agosti 2025Matangazo
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araqchi, saa kadhaa baada ya mataifa matatu ya Ulaya - Ujerumani, Ufaransa na Uingereza - kuanzisha mchakato wa siku 30 wa kuiwekea tena vikwazo Tehran. Nchi hizo zinaishutumu Iran kwa kushindwa kutimiza wajibu wake katika makubaliano yaliyofikiwa muongo mmoja uliopita kuhusu mpango wake wa nyuklia. Kwa upande wake Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya Kaja Kallas, amesema Ijumaa kuwa wiki kadhaa zijazo zinatoa nafasi ya kupata suluhisho juu ya mpango wa nyuklia wa Iran.