Iran iko tayari kwa diplomasia na nchi za magharibi
14 Julai 2025Matangazo
Kauli ya Qaempanah iliyochapishwa na gazeti la serikali la Iran Jumapili, imesisitiza kuwa diplomasia na hatua za kijeshi, zote zinaweza kutumika kama nyenzo za kudumisha haki katika taifa hilo.
Itakumbukwa kuwa baada ya mapigano ya siku 12 kati ya Israel na Iran kusimamishwa wiki kadhaa zilizopita, wanasiasa wa Iran na viongozi wa kijeshi walikataa mazungumzo na nchi za magharibi kuhusu mpango wa nyuklia wa nchi hiyo.
Kauli ya ofisi ya Rais wa Iran imetolewa siku moja baada ya Waziri wa mambo ya nje Abbas Araghchi kusema kuwa ushirikiano wa Tehran na Shirika la Kimataifa la kudhibiti nishati ya nyuklia (IAEA) haujavunjwa kabisa, tofauti na ripoti za awali.