Iran: Haina nia ya kujadili mpango wake wa nyuklia
27 Juni 2025Mzozo ulioibuka kati ya Israel na Iran, ulivuruga ratiba ya mazungumzo hayo kati ya Washinton na Tehran.
Hata hivyo Rais Donald Trump amesema Marekani itafanya majadiliano na Iran wiki ijayo na mjumbe wake maalum Steve Witkoff, akielezea matumaini yake juu ya kufikiwa makubaliano.
Lakini waziri wa mambo ya nchi za nje wa Iran Abbas Araghchi alipuuzilia mbali kauli hizo, akisema hakuna chochote kilichokubalika kufikia mkutano wa kujadili mpango wake wa nyklia.
Iran yasema haitasita kujibu mashambulizi yeyote
Kauli ya Araghchi inajiri baada ya bunge la Iran kupitisha muswada wa kusimamisha ushirikiano na Shirika la Kimataifa la Kudhibiti Nguvu za Atomiki, IAEA. Hatua hiyo bado inahitaji kuidhinishwa na Baraza la Juu la usalama wa Taifa nchini humo.