Iran yasema haiwezi kukatiza kabisa uhusiano wake na IAEA
20 Agosti 2025Matangazo
Aragchi ameongeza kuwa mabomba mapya ya nishati yanayotengenezwa kwa kutumia urani uliorutubishwa yanapaswa kuwekwa kwenye kinu cha nyuklia cha Bushehr nchini humo katika wiki zijazo, jambo ambalo litahitaji uwepo wa wakaguzi hao wa IAEA.
Iran itaendelea kufanya mazungumzo na Shirika la Kudhibiti Nishati ya Nyuklia la Umoja wa Mataifa
Katika mahojiano yaliyochapishwa leo, waziri huyo, ameliambia shirika la habari la serikali IRNA kwamba chini ya sheria iliyopitishwa na bunge, kurejea kwa wakaguzi hao kutawezekana kupitia uamuzi wa Baraza kuu la Usalama wa Kitaifa.
Matamshi hayo yanakuja takriban miezi miwili baada ya Iran kukatiza ushirikiano na shirika hilo laIAEAkufuatia vita vyake vya siku 12 na Israel mnamo mwezi Juni.