SiasaIran
Iran yapinga mazungumzo yenye sharti la kuacha urutubishaji
15 Julai 2025Matangazo
Hayo yameripotiwa na Shirika la Habari la Iran, IRNA, likimnukuu Ali Velayati ambaye ni mshauri mwandamizi wa Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei.
Afisa huyo amesema iwapo mazungumzo yoyote yatakayopendekezwa yatajumuisha sharti la kuitaka Iran iachane na urutubishaji madini ya Urani, nchi hiyo haitoshiriki.
Ametoa matamshi baada ya wizara ya mambo ya kigeni ya Iran kusema hadi sasa hakuna makubaliano yaliyofikiwa ya kufanyika mazungumzo mapya kati ya Iran na Marekani.
Mazungumzo ya awali kati ya pande hizo mbili yalivunjika mwezi Juni baada ya Israel kuishambulia Iran na Marekani kujiunga siku chache baadaye kuvishambulia vituo vya Iran vya kurutubishaji madini ya Urani.