Iran yapendekeza mazungumzo ya nyuklia na nchi za Ulaya
24 Aprili 2025Nchi hizo zenye nguvu Ulaya Ujerumani, Ufaransa na Uingereza zinazijulikana kama E3, mnamo Disemba zilisema kuwa ziko tayari kuiondolea Iran vikwazo vyote vya kimataifa ili kuizuia isiunde silaha ya nyuklia.
Iran iliyosema kwamba mpango wake wa nyuklia ni wa amani, inadai iko tayari kujadiliana kuhusu kusitishwa kwa sehemu za mpango wake wa nyuklia, ili iweze kuondolewa vikwazo vya kimataifa.
Iran imekuwa ikiendelea na mazungumzo kuhusu mpango wake wa nyuklia na utawala wa Rais Donald Trump wa Marekani na wachambuzi na wanadiplomasia wanasema, utawala huo wa Marekani umekuwa hauyashirikishi mataifa ya Ulaya kuhusiana na juhudi zake hizo.
Mnamo Jumatatu, Trump alisema Marekani ilikuwa na mazungumzo mazuri na Iran, siku mbili baada ya duru ya pili ya mazungumzo. Duru ya tatu itafanyika mjini Oman, Jumamosi ijayo.