Haki za binadamuIran
Iran yamnyonga aliyekutwa na hatia ya kuwa jasusi wa Israel
6 Agosti 2025Matangazo
Taarifa hizo ziliwezesha mauaji ya mwanasayansi wa nyuklia aliyeuawa mwezi Juni wakati wa mashambulizi ya Israel dhidi ya Jamhuri hiyo ya Kiislamu.
Hayo yameelezwa kwenye ripoti ya chombo cha habari cha mahakama kinachofahamika kama "Mizan" na kuongeza kuwa mtu huyo aliyefahamika kwa jina la Rouzbeh Vadi, alikuwa mfanyakazi katika moja ya "mashirika muhimu na nyeti" ya Iran, na kwamba alihatarisha usalama wa taifa hilo.
Kunyongwa kwa raia wa Iran baada ya kukutwa na hatia ya kuwa majasusi wa Israel, kumeongezeka maradufu mwaka huu, ambapo watu wanane walihukumiwa kifo katika miezi ya hivi karibuni.