Iran yakiri mapungufu ya kiusalama katika vita na Israel
17 Julai 2025Matangazo
Rais wa Iran Masoud Pezeshkian amekiri kwa mara ya kwanza kwamba nchi yake ilikuwa na mapungufu ya kiusalama katika vita vyake na Israel. Akizungumza katika kikao cha baraza la mawaziri mjini Tehran hivi leo,
Pezeshkian amesema mapungufu hayo yalidhihirika wakati wa vita na lazima yafanyiwe tathmini na kutafutiwa ufumbuzi.
Ukosoaji binafsi wa aina hii ni nadra sana nchini Iran.
Wakati wa vita va siku 12 kati ya Iran na Israel, makamanda wa vyeo vya juu wa Iran waliuliwa katika makazi yao binafsi na vituo vya kijeshi na vinu vya nyuklia kushambuliwa.