Iran yakataa mazungumzo ya moja kwa moja na Marekani
31 Machi 2025Matangazo
Kauli hiyo ya Pezeshkian ilikuwa jibu la kwanza rasmi la Tehran kwa barua ya Rais Donald Trump aliyomtumia kiongozi mkuu wa nchi hiyo, Ayatullah Ali Khamenei.
Kwenye jibu hilo lililotumwa kupitia serikali ya Oman, Rais Pezeshkian amesema kuwa upo uwezekano wa kufanyika mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na Washington.
Hata hivyo, mazungumzo kama hayo hayajaleta mafanikio yoyote, kwani Trump aliiondosha nchi yake kwenye makubaliano ya nyuklia kati ya Tehran na mataifa makubwa kwenye muhula wake wa kwanza wa urais mnamo mwaka 2018.
Trump, kwa upande wake, ametishia kuishambulia kijeshi Iran endapo Tehran haikusaini makubaliano na Washington.