Iran yakanusha ripoti ya kutaka kumfukuza balozi.
7 Machi 2004Matangazo
TEHERAN: Serikali ya Iran imekanusha ripoti ya gazeti la Iran kwamba ina niya ya kumfukuza Balozi wa Ujerumani mjini Teheran. Gazeti la mrengo wa kiasilia KEIHAN liliripoti kuwa Balozi Paul Freiherr von Maltzahn ametangazwa mtu asiyetakikana nchini humo baada ya kulaumiwa kwake kukutana na mwanasiasa wa upinzani wa Iran Ayatollah Hussein Ali Montaseri mwezi wa Januari na kutoa matamshi yanayoingilia mambo ya ndani ya Iran. Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani mjini Berlin, bado haikutoa tamshi lolote rasmi kuhusu ripoti hiyo.