Iran yajiandaa kukutana tena na Marekani kujadili Nyuklia
20 Aprili 2025Matangazo
Hata hivyo tayari vyombo vya habari vya Iran vinaionesha nchi hiyo kama ndiyo inayoshikilia nafasi yenye nguvu zaidi baada ya mazungumzo ya Jumamosi. Magazeti mengi ya Iranyameandika ripoti zinazoonesha kwamba Marekani imelegeza msimamo na inaihitaji zaidi nchi hiyo kwenye mazungumzo. Hadi sasa Iran inasema haijafanya mazungumzo ya moja kwa moja na Marekani katika duru mbili zilizokwishafanyika. Mazungumzo mengine kati ya wataalamu wa mataifa hayo mawili yatafanyika Jumatano nchini Oman.