Iran yadai Marekani yahujumu mazungumzo ya Nyuklia
10 Juni 2025Matangazo
Tuhuma za Iran zimetolewa siku chache kabla ya duru ya sita ya mazungumzo kuhusu nyuklia yaliyopangwa kufanyika pamoja na Marekani wiki hii.
Wabunge wa Iran kwenye taarifa yao wameilaumuMarekani kwamba haina haja ya mazungumzo hayo kabisa na badala yake imeweka mtego wa kulazimisha mapendekezo yake na kuchukuwa msimamo wa kutumia nguvu.
Rais Donald Trump jana Jumatatu alisema pande hizo mbili bado zinavutana kuhusu suala la urutubishaji madini ya urani katika ardhi ya Iran. Wabunge wa Iran wamesema suala hilo halina mjadala kwenye mazungumzo yanayohusu mpango wa nyuklia wa nchi yao.
Trump amesema mazungumzo yatafanyika Alkhamisi huku wizara ya mambo ya nje ya Iran ikisema yamepangwa kufanyika Jumapili nchini Oman.