MigogoroIran
Iran yaishutumu Israel kwa kuhujumu mazungumzo ya nyuklia
28 Aprili 2025Matangazo
Siku ya Jumapili, Netanyahu alisema makubaliano yoyote ya kweli kati ya Iran na Marekani ni yale ambayo yataondoa uwezo wa Iran wa kurutubisha madini ya urani kwa ajili ya silaha za nyuklia" na kuzuia utengenezwaji wa makombora.
Ametoa matamshi hayo siku moja baada ya wajumbe wa Iran na Marekani kukutana nchini Oman kwa awamu ya tatu ya mazungumzo ya ngazi ya juu kuhusu mpango wa nyuklia wa Tehran, huku pande zote mbili zikiripoti maendeleo.
Mazungumzo hayo yalianza Aprili 12, huku Tehran ikisisitiza yanapaswa kujikita kwenye suala la nyuklia tu na kuondolewa kwa vikwazo.