Iran yaishutumu Israel "kudhoofisha" mazungumzo ya nyuklia
21 Aprili 2025Matangazo
Esmail Baghai msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran amewambia waandishi habari Jumatatu kwamba kumekuweko na aina ya muungano ulioundwa ili kudhoofisha na kuvuruga mchakato wa kidiplomasia akisisitiza kuwa utawala wa Israel ndio kinara wa harakati hiyo. Kando ya Israel, Iran imesema wapo baadhi ya wanasiasa wa Marekani wanaopinga makubaliano kati ya nchi yao na Iran.
Gazeti la New York Times liliripoti Alhamisi kuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameizuia Israel kushambulia maeneo ya nyuklia nchini Iran kwa muda mfupi, kupisha hujudi za kidiplomasia.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameonya kuwa Israel kamwe haitaruhusu Iran kupata silaha za nyuklia, hata kama Washington itaendelea na mazungumzo.