Iran yaishambulia miji ya Haifa, Tel Aviv na Jerusalem
16 Juni 2025Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz, ameapa kwamba nchi hiyo itachukuwa hatua kali ya kujibu wimbi jipya la mashambulio yaliyofanywa na Iran katika miji ya Tel Aviv, Haifa na Jerusalem, usiku wa kuamkia leo.Hezbollah
Katz amesema kupitia ujumbe alioandika kwenye ukurasa wake wa X, kwamba wakaazi wa mji wa Tehran watalipa hivi karibuni, gharama ya kilichofanywa na serikali yao, huku akimuita kiongozi mkuu wa Iran, Ayatullah Ali Khamenei, kuwa dikteta aliyegeuka muuaji muoga, anayewalenga raia nchini Israel.
Jumla ya Waisraeli 23 wameuawa tangu Ijumaa kufuatia mashambulizi ya Iran.Mzozo wa Israel na Iran
Mashambulizi ya Iran ni ya kulipiza kisasi baada ya hapo Ijumaa, Israel kuanza kuyashambulia maeneo kadhaa nchini Iran, vikiwemo vinu vya nyuklia, miundombinu ya nishati, maji na hata makaazi ya raia, ambapo zaidi ya watu 220 wameuawa, wakiwemo wanawake na watoto, maafisa wakuu wa kijeshi pamoja na wanasayansi kadhaa.