Iran yaanza luteka ya kwanza tangu vita na Israel
21 Agosti 2025Kwa mujibu wa televisheni ya taifa, meli za kijeshi za Iran zimerusha makombora kuelekea Ghuba ya Oman na Bahari ya Hindi.
Ingawa mazoezi hayo ya kijeshi ni ya kawaida katika Jamhuri hiyo ya Kiislamu, mazoezi ya sasa yaliyopewa jina "Nguvu Endelevu 1404" yanafanyika wakati ambapo mamlaka nchini humo inajaribu kuonyesha uwezo wake wa kijeshi.
Iran inasisitiza kuwa iko tayari kukabiliana na kitisho chochote kutoka kwa Israel, hasa baada ya mifumo yake ya ulinzi wa anga na maeneo kadhaa ya nyuklia kuharibiwa katika vita hivyo viliyodumu siku 12.
Wakati huo huo, Iran imesitisha ushirikiano wake na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki, IAEA, ambalo limekuwa likifuatilia shughuli za nyuklia nchini humo, huku Tehran ikichakata madini ya urani hadi kufikia viwango vinavyoweza kutumika kutengeneza silaha.