MigogoroIran
Iran yamesema haina imani na usitishwaji vita wa Israel
30 Juni 2025Matangazo
Mkuu wa majeshi ya Iran Abdolrahim Mousavi alinukuliwa na televisheni ya taifa akisema kuna mashaka makubwa juu ya utii ulioonyeshwa na adui yao Israel, huku akionya kwamba wako tayari kujibu kwa nguvu" ikiwa watashambuliwa tena.
Anatoa matamsi haya siku sita baada ya usitishwaji wa mapigano uliotangazwa na Rais wa Marekani Donald Trump.
Vita baina ya mataifa hayo vilidumu kwa siku 12, baada ya Israel kuanza kuishambulia Iran kwa mabomu na kuwaua makamanda wakuu wa kijeshi na wanasayansi waandamizi wanaohusishwa na mpango wake wa nyuklia.
Tehran ilijibu kwa kuishambulia kwa makombora miji ya Israel.