Iran yaashiria kuwa tayari kwa mazungumzo na Trump
5 Februari 2025Matangazo
Waziri wa mambo ya nje wa Iran, Abbas Araghchi amesema serikali ya mjini Tehran inaweza kuwa tayari kwa mazungumzo na utawala wa Marekani unaoongozwa na rais Donald Trump.
Akizungumza pembezoni mwa mkutano wa baraza la mawaziri nchini Iran, Araghchi amesema ikiwa wasiwasi mkubwa uliopo ni kuhusu kuhakikisha Iran haitengenezi silaha za Nyuklia, basi hilo ni suala linaloweza kutatuliwa.
Soma pia: Urusi, Iran kusaini mkataba wa ushirikiano wa kimkakati
Trump alitowa agizo la rais hapo jana Jumanne linaloiamrisha serikali kuweka shinikizo kubwa zaidi dhidi ya Iran, linalojumuisha hatua za kuchukuliwa ikiwemo vikwazo vipya na kuviimarisha vikwazo vilivyopo.