SiasaAsia
Iran, Urusi, China kufanya luteka ya pamoja ya kijeshi
9 Machi 2025Matangazo
Shirika la habari la Tasnim la Iran limeripoti leo kuwa mazoezi hayo ya kijeshi yatafanyika katika bandari ya Chabahar iliyo kusini mashariki mwa Iran.
Nchi hizo tatu ambazo zina dhamira moja ya kukabiliana na kile wanachokitaja kama ushawishi mkubwa wa Marekani zimewahi kufanya mazoezi ya aina hiyo kwenye ukanda huo katika miaka ya hivi karibuni.
Soma zaidi: Urusi, Iran na China kufanya mazezi ya pamoja ya kijeshi
Kulingana na ripoti ya Tasnim, meli zenye silaha na kivita za China na Urusi pamoja na vikosi vya wanamaji vya jeshi la Iran na walinzi wa mapinduzi wanatarajiwa kushiriki. Azerbaijan, Afrika Kusini, Oman, Kazakhstan, Pakistan, Qatar, Iraq, Umoja wa Falme za Kiarabu na Sri Lanka zitashiriki kama waangalizi.