Iran kujadili mpango wake wa nyuklia na Ulaya
22 Agosti 2025Mataifa hayo matatu makubwa ya Ulaya awali yalitishia kuirejeshea Iran vikwazo ilivyowekewa na Umoja wa Mataifa, iwapo Jamhuri hiyo ya Kiislamu haitorejea tena katika meza ya mazungumzo kuhusu mpango wake huo wa nyuklia.
Mataifa hayo pamoja na Marekani wanadai kwamba Iran inatumia mpango huo kutengeneza silaha za nyklia, madai ambayo Iran inayakanusha vikali.
Iran yafanya luteka ya kwanza ya kijeshi tangu kukamilika kwa vita vya siku 12 na Israel
Iran iliyasimamisha kwa muda mazungumzo yake ya nyuklia na Marekani, baada ya taifa hilo pamoja na Israel kuishambulia katikati ya mwezi Juni.
Tangu wakati huo wachunguzi wa Shirika la Kimataifa la Kudhibiti Nguvu za Atomiki, IAEA, wameshindwa kufikia vinu vyake vya nyuklia licha ya mkuu wa shirika hilo Rafael Grossi kusema wachunguzi wake wanabakia kuwa muhimu na hawapaswi kunyimwa nafasi ya kuvikagua vinu hivyo.