Marekani, Iran zamaliza awamu ya nne ya mazungumzo Oman
11 Mei 2025Matangazo
Kwa upande wake Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Esmaeil Baqaei ameyaelezea majadiliano hayo kuwa yalikuwa magumu lakini yenye tija katika kutafuta njia sahihi za kuzishughulikia tofauti kati ya Tehran na Marekani kuhusu suala hilo.
Mazungumzo hayo yanalenga kudhibiti mpango wa nyuklia wa Iran ili Marekani iiondolee vikwazo vya kiuchumi. Kulingana na chanzo cha kuaminika kutoka upande wa Marekani, pande hizo mbili zimekubaliana kufanya mkutano mwingine hivi karibuni.