Iran na Marekani zajiandaa kukutana tena wiki hii
14 Aprili 2025Wizara ya mambo ya nje ya Iran imefahamisha kwamba mazungumzo mengine kuhusu mpango wake wa nyuklia na Marekani yamepangwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii na yataendelea kuwa mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja yakisimamiwa na Oman.
Iran imesema mazungumzo hayo yatahusu suala la nyuklia tu pamoja na kuondolewa kwa vikwazo na sio kingine.
Soma pia: Majadiliano kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran yanafanyika nchini OmanKauli hiyo ya wizara ya mambo ya nje ya Iran imetolewa jana Jumapili kufuatia duru ya mwanzo ya mazungumzo hayo yaliyofanyika Jumamosi nchini Oman.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Noel Barrot leo ameyakaribisha mazungumzo hayo kati ya mataifa hayo mawili lakini akasisitiza kwamba Ulaya itakuwa macho, kufuatilia ikiwa wasiwasi wake kuhusu usalama umezingatiwa.Soma pia: Iran yakataa mazungumzo ya moja kwa moja na Marekani
Wakati huo huo, taarifa zilizotolewa na msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran leo zinaonesha waziri wake, Abbas Araghchi, anatarajiwa kwenda Moscow kujadili suala hilo la nyuklia.