Iran na Marekani kuzungumzia mkataba wa nyuklia nchini Oman
11 Aprili 2025Matangazo
Iran imesema inaipa diplomasia fursa halisi na ya kweli katika mazungumzo ya nyuklia na Marekani licha ya shinikizo linalozidi kutoka kwa serikali ya mjini Washington, kuweka mazingira ya malumbano nchini Oman wikendi hii.
Mahasimu wa muda mrefu Iran na Marekani wanajiandaa kufanya mazungumzo mjini Muscat kesho Jumamosi yanayolenga kufikia mkataba wa nyuklia.
Jumatatu wiki hii rais wa Marekani Donald Trump alitoa tangazao la kushangaza kwamba utawala wake utafungua mazungumzo na Iran.
Mshauri wa cheo cha juu wa kiongozi mkuu wa kidini wa Iran Ayatollah Ali Khamenei amesema leo Ijumaa kabla mazungumzo ya Oman kwamba Iran inataka mkataba halisi wa haki na Marekani.