Iran: Mtetemeko wa ardhi wauwa watu 20,000
27 Desemba 2003Matangazo
TEHERAN: Huko BAM, mji ulioteketezwa karibu wote katika maafa ya mtetemeko mkubwa wa ardhi katika Iran, Kusini-Mashariki, watu wapatao 10,000 walibidi walale nje katika baridi kali hapo jana usiku baada ya kuteketezwa nyumba zao. Mpaka sasa hakuna takwimu za kutegemewa kuhusu kiwango cha watu waliouawa. Jopu la maafisa wanaoshauriana juu ya maafa hayo limesahihisha kile kiwango cha vifo 20,000 kilichotangazwa hapo awali. Wakati zikiendelea bado kazi za kuokoa watu hapawezi kuweko tarakimu za kutegemea, lilisemekana tangazo la jopo hilo. Lakini Waziri wa Mambo ya Ndani Jahanbash Chanshini alisema redioni, huenda kipimo cha uteketezaji wa balaa hilo kikawa hata kikubwa zaidi kupita makisio ya sasa. Shirika la Habari la Iran, IRNA limeripoti kuwa mjini Bam zimekwisha fukuliwa maiti 5,000. Inasemekana wamajeruhiwa baina ya watu 20,000 na 30,000.