Iran: Mazungumzo ya nyuklia na Ulaya yatafanyika Geneva
25 Agosti 2025Kituo cha televisheni cha taifa kimesema duru hiyo mpya ya mazungumzo ya ngazi ya manaibu waziri itahusisha mataifa hayo matatu yaliyosaini makubaliano ya Nyuklia ya 2015, pamoja na Umoja wa Ulaya. Duru iliyopita ya mazungumzo ilifanyika Istanbul, Julai 25.
Mazungumzo haya yanafanyika baada ya Iran kusitisha ushirikiano na Shirika la Kimataifa ya Udhibiti wa Nguvu za Atomiki, IAEA, kufuatia vita vya siku 12 na Israel mwezi Juni, ikilishutumu kwa kushindwa kulaani mashambulizi ya Israel na Marekani kwenye vituo vyake ya nyuklia.
Mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa hayo matatu ama E3 walitishia kutumia "utaratibu wa kurejesha vikwazo" ambao ni sehemu ya makubaliano ya nyuklia ya Iran ya mwaka 2015, isipokuwa Iran itakubali kudhibiti urutubishaji wa madini ya urani na kurejesha ushirikiano na wakaguzi wa IAEA.