Iran : Mashambulizi yatasitishwa Israel ikiacha uchokozi
15 Juni 2025Matangazo
Katika mkutano na wanadiplomasia wa kigeni, Araghchi ameongeza kuwa nchi yake inajitetea na kwamba utetezi wao ni halali kabisa na mashambulizi hayo ni jibu lao kwa uchokozi.
Pia amesema ikiwa uchokozi huo utakoma, mashambulizi yao pia yatasitishwa.
Netanyahu: Tutashambulia kila eneo la Iran
Araghchi pia amelishtumu Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kile alichokitaja kuwa hali ya kutojali kuhusiana na mashambulizi mabaya ya Israel dhidi ya jamhuri hiyo ya Kiislamu.
Waziri huyo amesema serikali za Magharibi zimeilaani Iran badala yaIsrael licha ya kuwa iliyochokozwa.