Iran: Mashambulizi ya Israel katika gereza la Evin yaua 71
29 Juni 2025Hayo yameelezwa na msemaji wa serikali Asghar Jahangir akiieleza Mahakama nchini humo. Jeshi la Israel lilifanya mashambulizi hayo siku ya Jumatatu katika gereza hilo ambalo kwa miongo kadhaa limekuwa na sifa mbaya ya ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi ya wapinzani wa kisiasa. Wanaharakati wa Iran wamelaani shambulizi hilo, wakisema lilihatarisha maisha ya wafungwa wa kisiasa.
Hayo yakiripotiwa, Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Kudhibiti Nishati ya Nyuklia (IAEA) Rafael Grossi amesema Iran inaweza kuanza tena kurutubisha madini yake ya urani ndani ya muda wa miezi kadhaa, licha ya madai ya Rais wa Marekani Donald Trump kwamba mpango wa nyuklia wa nchi hiyo umecheleweshwa kwa miaka miaka kadhaa kufuatia mashambulizi katika vituo vya mradi wa nyuklia vya Iran. Mpaka sasa athari za mashambulizi hayo hazijafahamika wazi.