Iran: Marekani imevuka "mstari mwekundu"
23 Juni 2025Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa, Amir Saeid Iravani, ameuambia mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba Marekani "imeamua kusambaratisha diplomasia," na kwamba jeshi la Iran litaamua "wakati, aina na ukubwa" wa "jibu sawia."
Marekani inadai kuwa mashambulizi yake vilisababisha uharibifu mkubwa, lakini haijawa wazi athari hizo ni kubwa kiasi gani. Waziri wa mambo ya nje wa Iran Abbas Araghchi amesafiri kuelekea mjini Moscow kuratibu na mshirika wake wa karibu Urusi juu ya hatua zitakazofuata.
Wakati makabiliano kati ya Israel na Iran yakiendelea, hofu ya kutokea mzozo mkubwa zaidi wa kikanda imezidi kuongezeka. Baadhi ya waangalizi wameonya pia kwamba mustakabali wa juhudi za kudhibiti kuenea kwa silaha za nyuklia kwa njia za amani upo hatarini kote duniani.