Iran kutia saini mkataba ziada wa marufuku ya kinyuklea
18 Desemba 2003Matangazo
VIENNA: Iran imetangaza kwamba alkhamisi ya leo itatia saini ile protokali ziada ya kukataza uenezaji wa silaha za kinyuklea. Sherehe hiyo ya utiaji saini mjini Vienna itahudhuriwa pia na Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Kinyuklea, IAEA, Mohammed El Baradei. Kwa kutia saini mkataba huo ziada, kwa mara ya kwanza Iran itaruhusu ukaguzi wa makini wa miradi yake ya kinyuklea kupitia wakaguzi wa kigeni.