Iran kurejea katika mazungumzo ya nyuklia
21 Julai 2025Matangazo
Televisheni ya kitaifa ya Iran, leo imemnukuu msemaji wa wizara ya mambo ya nje Esmail Baghai akisema kwa kujibu ombi la nchi za Ulaya, nchi hiyo imekubali kufanya duru mpya ya mazungumzo.
EU yatishia kuirejeshea Iran vikwazo isipofikia makubaliano ya nyuklia
Nchi hizo tatu za Ulaya zimeonya kuwa huenda vikwazo vikawekwa tena dhidi ya Iran iwapo haitarejea kwenye meza ya mazungumzo kuhusu mpango wake wanyuklia.
Iran na nchi hiyo tatu za Ulaya, zimefanya duru kadhaa za mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran na kuondolewa kwa vikwazo miongoni mwa masuala mengine tangu Septemba 2024.