Iran kumfukuza balozi wa Ujerumani.
7 Machi 2004Matangazo
TEHERAN:
Balozi wa Ujerumani nchini Iran, Oaul Freiherr
von Maltzahn karibuni atafukuzwa nchi kwa
mujibu wa taarifa ya gazeti la mrengo wa
kiasilia KEIHAN. Mwanadiplomasia huyo wa
Kijerumani analaumiwa kwamba baada ya kukutana
kwake na mwanasiasa wa upinzani wan
IranAyatollah Hussein Ali Montaseri mwezi wa
Januari alitoa matamshi yanayoingilia mambo ya
ndani ya Iran. Wizara ya Mambo ya Nje ya
Ujerumani mjini Berlin, bado haikutoa tamshi
lolote rasmi kuhusu ripoti hiyo.